Utoaji wa Magari Bandari ya Dar es Salaam • Yadi Binafsi ya In-Bond • Usafirishaji Mikoani
Malkia Cargo Wave Limited ni kampuni iliyosajiliwa rasmi na kupewa leseni ya forodha ya TRA kwa ajili ya kutoa na kusafirisha mizigo na magari, ikiwa na makao makuu yake Bandari ya Dar es Salaam, Tanzania.
Kuanzia gari moja binafsi toka Japan, Uingereza (UK), au Dubai, hadi magari ya makampuni na biashara, tunasimama na wewe hatua kwa hatua hadi funguo ziingie mkononi mwako salama.
Tumerahisisha mchakato mzima wa kutoa gari katika huduma nne kuu zilizo wazi na za uhakika.
Umeagiza gari toka Japan, UK au Dubai? Tunashughulikia taratibu zote za forodha Bandari ya Dar es Salaam, tunalipa ada zote, na kukuondolea usumbufu wote.
Huna hela ya kodi ya TRA kwa sasa? Epuka faini za bandari kwa kuhamishia gari lako kwenye yadi yetu salama chini ya forodha hadi utakapokuwa tayari kulipa.
Fahamu gharama zako mapema kabla meli haijafika. Tutumie invoice au export certificate, na wataalamu wetu watakupa mchanganuo kamili wa kodi ya TRA.
Unataka gari lako lifikishwe nyumbani kwako Dar es Salaam, kusafirishwa mikoani (Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya), au kuvuka mipaka kwenda nchi jirani.
Tunaondoa changamoto zote za bandari ili gari lako likufikie kwa amani, usalama na gharama nafuu.
Hakuna hofu ya kuibiwa betri, redio, taili ya akiba, au vioo. Tunafanya Physical Verification mara moja meli inaposhusha gari na kutoa ripoti rasmi getini.
Okoa mamilioni ya tozo za bandari. Tunahamisha gari lako kwenye yadi yetu chini ya bondi ya TRA ili ulipe kodi ukiwa tayari bila faini za kila siku.
Hesabu kamili ya kodi ya TRA na ada za bandari zinatolewa mapema na GePG Control Number kabla meli haijatua. Hakuna tozo zilizofichika.
Timu yetu yenye uzoefu inafanya kazi bandarini kila siku kushughulikia nyaraka, ukaguzi wa TBS, na kutoa gari kabla muda wa bure haujaisha.
Magari yetu maalum (car carriers) na madereva wazoefu wanakabidhi gari mlangoni kwako Arusha, Mwanza, Dodoma au Rwanda, Burundi, DRC na Zambia.
Fuatilia gari lako kwa namba ya B/L au Chassis wakati wowote kwenye mfumo wetu, ukisaidiwa na msaidizi wa AI masaa 24 kujibu maswali yako yote.
Kila kitu unachopaswa kufahamu kabla na baada ya gari lako kufika Bandari ya Dar es Salaam.
Tupo tayari kila wakati kujibu maswali yako na kukusaidia na gari lako.
Una swali kuhusu kuagiza gari, makadirio ya kodi ya TRA, au yadi yetu ya In-Bond? Wasiliana moja kwa moja na maafisa wetu wa forodha.
Jaza taarifa za gari lako na tutakupigia au kukutumia WhatsApp mchanganuo kamili.